Chumba 1 au 2 kwa wateja wa muda mrefu
Je, unatembelea Mwanza, mji uliozingirwa an miamba karibu na Ziwa Victoria, kwa ajili ya likizo, mafunzo, utafiti, kazi, au kumtunza mgonjwa hospitali ya Bugando? Nyakato Private Apartments zinakupa apartments za kujipikia kwa bei nafuu, ukae kwa raha kama uko nyumbani kwako, na kwa bei nafuu.
Apartments zetu ziko kwenye bustani kubwa yenye usalama wa hali ya juu, kwenye eneo tulivu na la amani. Utahisi uko nyumbani kila siku ya kukaa kwako kwetu, siyo kwa ughali bali kwa ukawaida na urahisi.
Tupo Nyakato Mahina, karibu na stendi maarufu ya mabasi ya Buzuruga, kilomita 5 tu kutoka katikati ya jiji la Mwanza. Usafiri wa umma, maduka, baa na huduma nyingine nyingi zinapatikana karibu na nyumbani , na hivyo kurahisisha sana maisha yako.
Apartments Zetu
Tunatoa apartments zilizo na fanicha (furnished) na zisizo na fanicha (unfurnished) kwa wateja wa muda mrefu kama zilivyo nyumba za kupanga za kawaida. Kila apartment inajumuisha:
- Chumba 1 au 2 chenye kitanda kikubwa cha futi 5x6
- Sebule
- Jiko dogo lenye jiko la gesi
- Bafu lenye choo cha kukaa na maji ya moto ya kuoga
- TV na king'amuzi cha Satellite
Bei zetu nafuu
Apartment ya Chumba 1 Yenye Fanicha
- Kwa Wiki: TSh 119,000 (watu 1-2)
- Kwa Mwezi (Malipo ya Mapema): TSh 450,000 (punguzo la 13%)
- Miezi Miwili (Malipo ya Mapema): TSh 400,000 (punguzo la 23%)
Ofa Maalum (Novemba 2024 - Januari 2025):
-
- Kwa Mwezi (Malipo ya Mapema): TSh 350,000
- Miezi Miwili (Malipo ya Mapema): TSh 320,000
Apartment ya Vyumba 2 Yenye Fanicha
- Kwa Wiki: TSh 160,000 (watu 1-4)
- Kwa Mwezi (Malipo ya Mapema): TSh 600,000 (punguzo la 16%)
- Miezi Miwili (Malipo ya Mapema): TSh 500,000 (punguzo la 28%)
Bei za apartments zisizo na fanicha zinapatikana kwa maombi.
Kumbuka: Kwa viwango vya punguzo, gharama za umeme na kifurushi cha TV havijumuishwi. Vinginevyo, tunatoa kifurushi cha Azam PURE (channel 85+) kwa TSh 19,000 kwa mwezi. Kwa kukaa kwa mwezi mmoja au zaidi, tunagharamia kifurushi cha TV.
Huduma za Apartments
- Maegesho ya gari ya bure kwenye eneo la nyumba
- Kibanda cha kupumzika au kufanya kazi nje
- Matanki ya maji kwa huduma ya maji ya uhakika
- Mazingira rafiki kwa familia na watoto
- Huduma za usafi, kufua, na kupika zinapatikana kwa maombi
- Mita ya umeme ya LUKU ili kila mtu aangalie matumizi yake
Wasiliana nasi!
Piga simu au tutembelee kwenye Instagram: #MwanzaCityApartments